Urusi yaonya Marekani kuhusu makombora

Urusi inaweza kulipiza kisasi iwapo Marekani itaendelea kusisitiza kujenga mitambo ya makombora ya kujihami huko Ulaya.

Rais Medvedev amesema iwapo Marekani itatekeleza mpango wake huo, Urusi nayo itaweka makombora yake katika eneo la Kaliningrad linalopakana na Poland.

Mpango wa Marekani wa kuwa na makombora ya kujihami barani Ulaya uliasisiwa wakati wa uongozi wa aliyekuwa rais wa Marekani George W. Bush ambao uliathiri vikali uhusiano kati ya Marekani na Urusi.

Rais wa Marekani Barrack Obama ameondoa baadhi ya vipengele tata kwenye mpango huo lakini Urusi imesema bado ina wasiwasi kuhusu mpango huo.