Rais Saleh atia saini mkataba kujiuzulu

Maandamano na ghasia zinazoyakumba mataifa ya kiarabu yamemfanya rais wa Yemen Ali Abdallah Saleh kusalimu amri baada ya kutawala Yemen kwa zaidi ya miaka 30.

Rais huyo ametia saini makubaliano ya kumuachia naibu wake mamlaka yote na uchaguzi wa urais kufanywa haraka.

Katika makubaliano hayo Rais Saleh pia atapatiwa kinga ya kutoshitakiwa mahakamani kwa makosa anayodaiwa kufanya akiwa rais.