Syria yaijibu Jumuiya ya Kiarabu

Serikali ya Syria imetoa kwa kile ilichosema kauli njema kwa mpango wa amani wa jumuiya ya nchi za kiarabu.

Siku moja baada ya muda wa mwisho uliotolewa kwa Damascus kutia saini kumalizika, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Syria amesema nchi hiyo imeonyesha ipo tayari kutia saini makubaliano ya kuruhusu waangalizi.

Lakini amesema Syria imetaka makubaliano hayo yatiwe saini mjini Damascus, na si kwenye makao makuu ya jumuiya hiyo huko Cairo.

Amesema Syria imetaka vikwazo vyote vilivyotolewa na jumuiya ya nchi hizo za kiarabu vifutwe baada ya kutia saini makubaliano hayo.