Ufaransa na Ujerumani zakubaliana

Viongozi wa Ufaransa na Ujerumani wamesema wamekubaliana juu ya hatua zinazotakiwa kuimarisha ukanda wa Ulaya.

Katika mkutano huko Paris, Nicolas Sarkozy na Angela Merkel wamesema wanataka makubaliano mapya.

Wamesema watakubali itakayosainiwa na wanachama wa ukanda huo iwapo hawatoungwa mkono na muungano mzima wa Ulaya.

Wamekubaliana kuwa Ulaya itekeleze sheria ya kuwepo asilimia tatu kwenye nakisi za taifa, na kila nchi ikubaliane na bajeti yenye uwiano sawa.