Bi Clinton ziarani Burma

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Bi Hilary Clinton yuko nchini Burma kwa ziara ya kihistoria katika nchi iliyotengwa kidiplomasia.

Hii ni ziara ya kwanza kwa waziri wa masuala ya kigeni wa Marekani kuitembelea Burma tangu mwaka 1955.

Serikali mpya ya kiraia ya Burma inayowajumuisha viongozi wa zamani wa serikali ya kijeshi imefanya mageuzi kadhaa.

Bi Clinton pia anatarajiwa kufanya mazungumzo na kiongozi maarufu wa wa upinzani nchini humo Bi Aung San Suu Kyi.