Uingereza yashiniza vikwazo dhidi ya Iran

Ubalozi was Iran nchini Uingereza Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Ubalozi wa Iran nchini Uingereza

Waziri wa mambo ya nje Uingereza, William Hague anasema, anashinikiza Iran iwekewe vikwazo zaidi katika mkutano wa leo wa mawaziri wa umoja wa ulaya.

Amesema hayo siku mbili baada ya waandamanaji kuvamia ubalozi wa Uingereza nchini Iran.

Akizungumza mjini Brussels, Bw Hague ambaye aliamuru kufungwa kwa ubalozi wa Iran nchini Uingereza.

anasema anatumai kuwa mawaziri watashirikiana kuiwekea shinikizo la kiuchumi Iran.