Marekani yasema ''Boko Haram'' ni tisho

Mashambulio ya Boko Haram
Image caption Mashambulio ya Boko Haram kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Abuja

Ripoti ya bunge la Congress la Marekani imelitaja kundi la kiislam la Boko Haram, kama tishio kwa usalama wa Marekani.

Mwenyekiti wa kamati iliyoandika ripoti hiyo, Patrick Meehan, ameiambia BBC kuwa Marekani inapaswa kuongeza mbinu za ujasusi nchini Nigeria na kuimarisha uhusiano wake na idara ya usalama ya Nigeria.

Kundi hilo la Boko Haram limekuwa likifanya mashambulio nchini Nigeria, likiwemo shambulio lililosababisha mauaji ya takriban watu 150 kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa.

Marekani inasema huenda kundi hilo linaimarisha uhusiano na makundi mengine ya kigaidi kama vile al-shabaab.