FIFA Yasusiwa kwa ufisadi

Sepp Blatter Haki miliki ya picha BBC World Service
Image caption Rais wa shirikisho la soka duniani Sepp Blatter

Shirika la kupambana na rushwa ambalo limekuwa likilishauri shirikisho la soka duniani FIFA baada ya shirikisho hilo kugubikwa na kashfa za rushwa na ufisadi, limevunja ushirikiano nalo.

Shirika hilo la Transparency International limesema halikufurahishwa na FIFA kupuuza mapendekezo yake ya msingi kwa shirikisho hilo.

Transparency International liliondoa msaada wake wa ushauri baada ya kuhoji mfumo huru wa uchunguzi katika kashfa zinazoikabili FIFA.

FIFA imekataa kuzungumzia suala la kuvunjika kwa uhusiano baina yake na Transparency International.