Chansela Merkel azungumzia uchumi Ulaya

Chansela Angela Merkel na Rais Nicolas Sarkozy Haki miliki ya picha Getty
Image caption Chansela wa Ujerumani Angela Merkel na Rais wa Ufaransa Nicolas Sarkozy

Kiongozi wa Ujerumani, Chansela, Angela Merkel, amesema juhudi za kupata suluhu la kudumu kwa matatizo ya kiuchumi yanayokabili mataifa yanayotumia sarafu ya Euro zitachukua miaka mingi.

Akilihutubia bunge la Ujerumani Bi Merkel amesema muungano wa ulaya utakaoratibu masuala ya fedha utabuniwa na utakuwa na jukumu la kuratibu matumizi ya bajeti katika mataifa yanayotumia sarafu ya Euro.

Ujerumani na Ufaransa zinatafuta mikakati itakayosaidia kupata suluhisho la matatizo ya uchumi barani Ulaya.

Rais wa Ufaransa , Nicolas Sarkozy, amesema atakutana na Bi Angela Merkel, Jumatatu ijayo, kutangaza mpango wa pamoja wa kulinda mfumo wa baadaye wa uchumi barani Ulaya.