Uhusiano wa Iran na Uingereza wayumba

Ubalozi wa Uingereza mjini Tehran
Image caption Uvamizi dhidi ya ubalozi wa Uingereza mjini Tehran

Wafanyakazi wanaofanyia kazi kwenye ubalozi wa Iran mjini London lazima waondoke kufikia Ijumaa mchana.

Wanatakiwa kuondoka nchini humo saa nane za mchana kwa saa za Uingereza baada ya amri hiyo kutolerwa na waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza William Hague, baada ya ubalozi wa Uingereza mjini Tehran kuvamiwa.

Mamia ya waandamanaji waliuvamia ubalozi wa Uingereza mjini Tehran Junanne, kufuatia uamuzi wa Uingereza kuiwekea vikwazo zaidi Iran kuhusu mpango wake wa nuklia.

Vikwazo hivyo vimelifanya bunge la Iran kupunguza ushirikiano na Uingereza.

"Kama nchi yoyote haitaweza kutuwezesha kufanya kazi kwenye ardhi yake, wasitarajie sisi turuhusu ubalozi wao kufanyia kazi hapa'', Bwana Hague aliwaambia wabunge Jumatano.