Matokeo ya awali Congo yatarajiwa leo

Tume ya uchaguzi katika nchi ya Kidemokrasi ya Congo inatarajiwa kutangaza matokeo ya awali ya uchaguzi mkuu uliofanyika wiki iliopita baadaye hii leo.

Matokeo ya mapema yanaonyesha rais wa sasa Joseph Kabila akimtangulia mpinzani wake mkuu Etienne Tshisekedi.

Hata hivyo upinzani umesema hautakubali matokeo iwapo rais Kabila atachaguliwa tena.

Waangalizi wa kimataifa wamesema uchaguzi huo umeendeshwa vizuri kwa jumla licha ya malumbano kati ya wafuasi wa viongozi mbali mbali na pia madai ya kuwepo kwa udanganyifu.