Chanjo ya Ebola huenda imepatikana.

Wanasayansi wametengeneza chanjo inayokinga panya kupata virusi vya Ebola.

Ebola iligunduliwa mwaka wa 1976, na inauwa zaidi ya asilimia 90% ya watu wanaoambukizwa. Matokeo ya chanjo hiyo yalichapishwa kwenye jarida moja la masuala ya afya la Proceedings of National Academy of Sciences.

Ingawa idadi ya watu wanaoambukizwa ugonjwa huo kila mwaka ni ndogo, athari zake huwa zinasambaa kwa haraka na inahofiwa kuwa huenda virusi hivyo vikatumika na magaidi kama silaha.

Chanjo hii mpya inakinga thabiti kwa hadi asilimia 80% kwa panya dhidi ya maradhi hayo na pia ina uwezo wa kustahimili joto jingi na baridi kulingana na mwanasayansi Charles Arntzen kutoka chuo kikuu cha Arizona ambaye alihusika katika utafiti wake.