Makabiliano yazuka Sudan Kusini

Serikali ya Sudan Kusini imesema majeshi yake yamekabiliana na wanajeshi kutoka Sudan ambao inawashtumu kwa kuingia Sudan Kusini mwishoni mwa juma.

Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini ameiambia BBC kuwa kitendo hicho hakiwezi kuvumiliwa na kuwa wanajeshi hao watalazimishwa kuondoka.

Ameshtumu jeshi la Sudan kwa kutumia zana zinazolenga mbali kushambulia Sudan kusini na kusababisha takriban watu elfu tano kuhama eneo hilo.

Sudan kusini imetoa wito kwa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuingilia kati kuzima mashambulizi kutoka Sudan.