UN yasitisha kandarasi za ndege za kirusi

Mikataba ya kampuni mbili za kirusi za uchukuzi wa ndege zimesimamishwa kuendelea na shughuli zake katika mataifa ya Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na Sudan.

Kampuni hizo zilikuwa zimepewa kandarasi na Umoja wa Mataifa nchini Sudan na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo.

Hatua hii imechukuliwa kufuatia madai kuwa wafanyakazi wake wamekuwa wakiwadhulumu kimapenzi wakaazi wa mataifa hayo.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa katika idara ya harakati za kudumisha amani amesema kuwa uchunguzi kwa wafanyakazi wa kampuni za ndege za Utair na Nefteygansk umegundua kuwa madai mengine yalikuwa kweli.

Wafanyakazi waliohusika katika kashfa hiyo tayari wamefutwa kazi.