Rais wa Zimbabwe ataka urais 2012

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, anatarajiwa kuomba chama chake cha ZANU-PF kumuunga mkono wakati wa mkutano wa kila mwaka wa chama hicho utakapofanyika leo, Alhamisi.

Afya ya rais huyo mwenye umri wa miaka 87 inazidi kuzorota lakini anataka kugombea urais mwaka 2012.

Wanahabari wanasema baadhi ya wajumbe wa chama cha ZANU-PF wana wasiwasi kuhusu afya ya rais Mugabe.

Serikali ya muungano iliyopo sasa imeimarisha taifa hilo kwa kiasi kikubwa lakini kuna wengi wanaoamini kwamba uchaguzi huenda ukaleta malumbano hasa kwa sababu bado hakuna katika mpya.