Matokeo ya urais DRC ni leo

Tume ya uchaguzi katika Demokrasia ya Congo imesema itatangaza matokeo ya uchaguzi mkuu katika muda wa masaa machache yajayo.

Kutangazwa kwa mshindi kuliahirishwa huku tume hiyo ikisema inataka muda zaidi ili kuhakikisha kura kutoka maeneo yote ya nchi hiyo zimekusanywa na kuhesabiwa.

Hali ya taharuki inazidi kutanda katika mji mkuu wa Kinshasa huku wafuasi wa rais Joseph Kabila na wale wa kiongozi wa upinzani Etienne Tshisekedi wakisubiri kwa hamu matokeo hayo.

Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa amesema kumekuwa na makabiliano kati ya maafisa wa usalama ambao wanaunga mkono wagombea tofauti.