Mataifa ya Ulaya yaafikiana

Mataifa ishirini na matatu ya Ulaya yameafikiana kuhusu mkataba mpya wa kuratibu masuala ya kifedha kwa minajili ya kurejesha imani ya kiuchumi katika mataifa yanayotumia sarafu ya Euro yanayokabiliwa na matatizo ya madeni.

Hata hivyo juhudi za kuyashawishi mataifa yote ishirini na saba wanachama wa Muungano wa Ulaya ikiwemo Uingereza kujumuishwa katika makubaliano hayo zimegonga mwamba.

Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron ameambia waandishi wa habari kwamba mkataba uliotiwa saini na mataifa mengine ya Ulaya haukuridhisha taifa lake na ndio maana hakutia saini.