Burma:Suu Kyi akubaliwa kusajili chama

Kiongozi wa upinzani nchini Burma Aung San Suu Kyi amepewa idhini rasmi na utawala wa kijeshi nchini humo kusajili chama chake.

Chama cha Bi Suu Kyi kinachojulikana kama the National League for Democracy (NLD) - kilipigwa marufuku baada ya kususia uchaguzi wa mwaka uliopita ambao kilisema haukuwa huru na wa demokrasia.

Lakini serikali ya Burma imeanza kutekeleza mabadiliko ya kisiasa nchini humo.

Wiki iliyopita chama hicho kilisema kitawaweka wagombea katika chaguzi ndogo zote arobaini na nane zinazokuja katika miezi ijayo huku Aung San Suu Kyi akigombea kiti cha ubunge katika mji wa Kawhmu kusini mwa Rangoon.