Canada yajiondoa katika mwafaka wa Kyoto

Uchina imeelezea masikitiko yake kuhusiana na uamuzi wa Canada kujiondoa katika Mwafaka wa Kyoto kuhusu kupunguza viwango vya gesi inayochafua mazingira duniani.

Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini uchina amesema hatua hiyo ya Canada inakwenda kinyume na juhudi za jamii ya kimataifa.

Canada imekuwa nchi ya kwanza kujiondoa rasmi katika mwafaka huo, siku moja baada ya mazungumzo ya kimataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa mjini Durban kukamilika bila makubaliano kuhusu mwafaka mpya utakaochukuwa pahala pa mwafaka wa Kyoto.

Mwafaka wa Kyoto unamalizika mwishoni mwa mwaka ujao.