Leon Panetta azuru Djibouti

Waziri wa Ulinzi wa Marekani Leon Panetta anafanya ziara rasmi nchini Djibouti.

Jeshi la Marekani lina kituo nchini Djibouti na waziri huyo wa Uliunzi amezungumzia umuhimu wa vita dhidi ya Al Qaeda na makundi washirika kutoka Yemen na Somalia.

Baada ya kuwasili Djibouti, Leon Panetta, amesema nchi kama Somalia na Yemen zimekuwa zikilengwa sana na Marekani katika vita dhidi ya Ugaidi.

Ndege za kivita zisizokuwa na rubani zimekuwa zikielekezwa nchini Somalia kulenga kundi la wanamgambo wa kiislam la, Al Shabab.