Marais wa kanda ya Maziwa Makuu wakutana

MKUTANO wa nne wa kikao cha kawaida cha marais wa kanda ya Maziwa makuu umeanza nchini Uganda.

Marais wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na Yoweri Museveni wa Uganda, Jakaya Kikwete wa Tanzania, Mwai kibaki wa Kenya, Pierre Nkurunziza wa Burundi pamoja na Michael Sata wa Zambia.

Mkutano huo unazungumzia masuala ya usalama katika kanda maziwa makuu na pia suala la unyanyasaji wa kijinsia katika kanda hiyo.