Waasi wapigana na serikali Syria

Mapigano yamezuka kati ya wanajeshi walioasi na wale wa serikali kusini mwa syria. Shirika la kutetea haki za kibinadamu lenye makao yake mjini London, Syrian Observatory for Human Rights, limesema kuwa wanajeshi waasi waliwaua takriban wanajeshi wa serikali 27 katika mapigano yaliyozuka katika mkoa wa Deraa mapema leo.

Hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu watu waliojeruhiwa na taarifa hizo bado hazijathibitishwa.

Wanajeshi wa serikali wamekuwa wakishambuliwa kwa siku ya tatu sasa.

Makundi ya kutetea haki za kibinadamu yanasema jeshi la Syria limewauwa takriban watu kumi na saba siku ya Jumatano, kumi kati yao wakiuwawa katika eneo la Hama.