Kim Jong-il afariki dunia

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-il, mwenye umri wa miaka 69, amefariki. Kifo chake kimetangazwa na televisheni ya taifa hilo.

Kufuatia kifo cha kiongozi huyo, habari kutoka Korea Kusini zinasema kuwa taifa hilo jirani limeweka wanajeshi wake katika hali ya tahadhari.

Shirika la habari la kifaifa la korea Kusini (yonhap) limesema kuwa Serikali imeitisha mkutano wa Baraza Kuu la Usalama.

Nako Nchini Japan, msemaji wa Serikali amedokeza kuwa Waziri Mkuu ameunda tume maalumu ya kushughulikia maswala ya Korea Kaskazini.