Uingereza yatengana na Jumuiya ya Ulaya

Kwa mara nyingine tena Uingereza imejitenga na mataifa mengine ya Ulaya yanayotumia sarafu ya Yuro.

Tayari serikali ilikuwa imetangaza kuwa haitachangia jumla ya Yuro Bilioni mia mbili ambazo mataifa wanachama wa Jumuiya ya Ulaya wanaotumia Yuro wameahidi kutoa kwa Benki ya Dunia.

Walitaka pesa hizo zipatikane ili IMF nayo ikopeshe mataifa ya Ulaya ambayo kwa wakati huu yanapambana katika juhudi za kulipa madeni yao.

Kutokana na uamuzi huo wa Uingereza Mawaziri wa Kigeni kutoka mataifa hayo ya Ulaya sasa inawabidi wakadirie mpango wao kwa kiasi kidogo zaidi.