Ufilipino: Mafuriko ni janga la Kitaifa

Rais wa Ufilipino Benigno Aquino ametangaza mafuriko kuwa janga la kitaifa baada ya mvua za masika kuua karibu watu 1,000.

Kimbunga cha Washi kimepiga eneo la kusini katika kisiwa cha Mindanao na kulizunguka eneo hilo mwishoni mwa wiki.

Alipolitembelea eneo hilo, Bw Aquino aliwahakikishia waathirika kuwa serikali itakuwepo kuwasaidia lakini ilikiri uwezekano wa kuwepo makosa.

Baadhi ya mamlaka zimeanza kufanya mazishi ya watu wengi lakini wamepingwa na baadhi ya ndugu wa marehemu.

Mashirika ya misaada yanajaribu kupeleka vyakula, maji, dawa na miili ya kuhifadhia miili, lakini barabara zilizoharibiwa vibaya zinazuia juhudi za kuwafikia waathirika katika vijiji..