Askari wauawa wakikimbia Jeshi Syria

Imebadilishwa: 20 Disemba, 2011 - Saa 13:54 GMT

Wanajeshi wengi waliokimbia jeshi wameuawa na vikosi vya Syria wakati wakijaribu kutoroka kambi zao na kujiunga na waandamanaji, ripoti zinasema.

Makundi ya wanaharakati yalisema zaidi ya askari 70 waliokimbia walipigwa risasi katika jimbo la kaskazini magharibi la Idlib.

Walisema idadi ya vifo vya Jumatatu nchi nzima inaweza kuzidi 110 – kama ni kweli itafanya kuwa moja ya siku ya mauaji makubwa katika ghasia hizo.

Awali Damascus ilikubali mpango wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu kuruhusu waangalizi kuingia nchini.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Walid Muallem alisema Jumuiya hiyo imekubali marekebisho ambayo Damascus iliyataka.

Taarifa zinazohusiana

BBC © 2014 Ilani: BBC haihusiki na yaliyoandikwa na tovuti za nje ya BBC.

Ukurasa huu unaonekana vyema kwa kivinjari cha kisasa kikiwa na laha mtindo (CSS).Wakati unaweza kuona yaliyomo katika ukurasa huu kwa kivinjari ulichonacho, hautaweza kufaidi kuona kila kitu vizuri. Tafadhali zingatia uwezekano wa kuboresha progaramu ya kivinjari au kuwezesha laha mtindo (CSS) endapo unaweza kufanya hivyo.