Matiti pandikizi kuondolewa Ufaransa

Mamlaka nchini Ufaransa zinatarajia kuwaomba wanawake wapatao 30,000 waliopandikiziwa matiti yenye hitilafu kuondolewa tena, taarifa zinasema.

Kuna wasiwasi kuwa matiti hayo ya kupandikizwa yaliyosambazwa na kampuni ya Poly Implant Prothese (PIP) yalikuwa na athari za kiafya, kwa mujibu wa gazeti la Liberation.

PIP ilikutwa mwaka jana imetumia ‘silicone gel’ ambayo haijathibitishwa na ilisababisha kiwango cha juu cha upasukaji.

Serikali ya Ufaransa imeunda kamati maalum ya kuchunguza suala hilo.

"Hatuna budi kuyaondoa matiti yote haya ya kupandikiza," Dr Laurent Lantieri, bingwa wa upasuaji wa kubadilisha viuongo, aliye kwenye kamati aliliambia gazeti la Libaration. "Tumekumbana na mgogoro wa kiafya unaohusishwa na ufisadi."