Kazakhstan yaomba msaada wa uchunguzi

Serikali ya Kazakhstan imetoa wito kwa Umoja wa Mataifa kusaidia katika uchunguzi baada ya makabiliano ya juma lililopita ambapo watu 16 walikufa.

Serikali kwa upande wake imeahidi kuwa itafanya uchunguzi wa huru kuhusiana na ghasia hizo.

Polisi wanasema walifyatua risasi baada ya kushambuliwa na wafanyikazi wa mafuta ambao walikuwa wamefutwa. Wafanyikazi hao walikuwa wakifanya maandamanano kwa miezi kadhaa.