Ruhusu pesa Somalia - Mashirika

Mashirika mawili ya kutoa misaada kwa Somalia nchini Marekani imetoa wito kwa Benki moja ya Marekani isikatize huduma ya kutuma pesa kwa wananchi wa Somalia

Taifa hilo kwa sasa lina zaidi ya watu robo milioni wanaokabiliwa na upungufu mkubwa wa chakula.

Benki hiyo ambayo haikutajwa imesema kuwa itasimamisha shughuli zake za kuhamishia pesa Somalia ili kujiepusha kuvunja sheria za kupambana na ugaidi kifedha.

Mashirika hayo mawili ni Shirika la Oxfam nchini Marekani na Tume ya Wakimbizi ya Marekani.