Eric Cantona agombea urais Ufaransa

Mwanasoka mkongwe wa Ufaransa Eric Cantona anajaribu kutafuta idadi ya kutosha ya kuungwa mkono kwa ajili ya kugombea urais.

Amewaandikia mameya wa Ufaransa akitafuta saini 500 ambazo mgombea yeyote wa urais anahitaji nchini humo.

Hata hivyo, wachambuzi wamesema hatua yake hiyo huenda ikawa ni jaribio tu la kuwavutia watu na ajenda yake ya sasa, ambayo ni makazi duni.

Akiwa anajulikana kwa uhodari wake uwanjani, Cantona aliwahi kujihusisha kwenye kuigiza na siasa, mafaniko yakiwa si mazuri sana.