Kiongozi awatisha 'Wagambia wavivu'

Yahya Jammeh ameapishwa kwa awamu ya nne kuwa rais wa Gambia na ameahidi "kuwafukuza kazi asilimia 82" ya wafanyakazi, akiwashutumu kuwa wavivu.

Kiongozi huyo aliyekuwa afisa wa jeshi aliahidi "kuwa na hatari zaidi kuliko nilivyokuwa nikivaa sare".

Pia amesema anataka kugeuza nchi hiyo ndogo iliyopo Afrika Magharibi kuwa na "nguvu kubwa ya kiuchumi" katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Rais Jammeh aliingia madarakani mwaka 1994 lakini alichaguliwa tena mwezi Desemba katika uchaguzi uliokosolewa sana.