Madaktari 'feki' wakamatwa India

Polisi katika jimbo la Bihar nchini India wamewakamata watu watatu waliojifanya madaktari, ambao wamewafanyia upasuaji 'feki' wanawake 53 wa kufunga kizazi katika kipindi cha saa mbili.

Upasuaji huo ulifanyika uwanjani na bila kutumia nusu kaputi, kwenye wilaya ya Araria.

Washukiwa hao watatu walikamatwa wakihisiwa "kufanya upasuaji bila ridhaa na kinyume cha sheria," polisi walisema.

Baadhi ya wanawake hao waliathirika kutokana na upasuaji huo na hivyo kupelekwa hospitalini.