Mwanasiasa wa Ireland akutwa na hatia

Mwanasiasa wa Republican wa Ireland ya Kaskazini amepatikana na hatia ya kuwaua wanajeshi wawili wa Uingereza nje ya kituo cha kijeshi, takriban miaka mitatu iliyopita.

Brian Shivers amepatikana na hatia ya kuwafyatulia risasi wanajeshi hao walipokuwa wakipokea Pizza kwenye lango la kuingia kituoni hapo huko Antrim.

Mtu wa pili anayesemakana kuwa ni mwanachama wa Kundi la Real I.R.A Colin Duffy hakupatikana na hatia ya mauaji hayo.

Wanajeshi hao wawili wa Uingereza waliuawa katika mkesha wa siku ambayo walikuwa wapelekwe Afghanistan.