Beyonce ajifungua mtoto wa kike

Beyonce na Jay-Z wamepata mtoto wao wa kwanza, kulingana na ripoti kutoka Marekani

Taarifa hizo zilitolewa mara ya kwanza kwenye mitandao mbalimbali ya watu maarufu na kuthibitishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter na marafiki wa wasanii hao maarufu, akiwemo Rihanna na Gwyneth Paltrow.

Taarifa zinasema mtoto huyo wa kike, Blue Ivy Carter, alizaliwa kwa njia ya upasuaji siku ya Jumamosi.

Hata hivyo, mpaka sasa wanandoa hao hawajathibitisha rasmi kwa kauli yao kuzaliwa kwa mtoto huyo.