Tajiri wa Misri ashtakiwa kwa kukufuru

Mmoja wa matajiri wa Misri na mfanyabiashara maarufu, Naguib Sawiris, anatarajiwa kukabiliana na mashtaka ya kutoa kashfa dhidi ya Uislamu.

Bw Sawiris ambaye ni mkristo wa madhehebu ya Copti, yuko matatani kwa kuweka kibonzo cha Mickey na Minnie Mouse wakiwa wamevaa nguo za kiarabu kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.

Aliomba radhi baada ya kibonzo chake hicho kusambazwa kwenye twitter mwaka jana, lakini mawakili wengi wametoa malalamiko rasmi kupinga kitendo chake hicho.

Kumekuwa na wito pia wa kugomea mtandao wa simu wa MobilNil unaoendeshwa na Bw Sawiris.