Besigye wa Uganda aachia ngazi

Kiongozi mkuu wa upinzani Uganda, Kiiza Besigye, ametangaza kuachia ngazi mapema kama kiongozi wa chama cha Forum for Democratic Change.

Dr Besigye alisema anataka kujiunga na harakati pana zaidi za kijamii zinazoipa changamoto serikali ya Rais Yoweri Museveni.

Amepuuzilia mbali pendekezo kuwa kuondoka kwake kutauacha upinzani bila uongozi thabit.

Mwaka jana Dr Besigye alikamtwa mara kwa mara kwa kujihusisha na maandamano ya kuipinga serikali.