Upinzani Syria wataka raia walindwe

Kiongozi wa kundi kuu la upinzani nchini Syria ameutaka ujumbe wa muungano wa mataifa ya kiarabu uliopo nchini humo kukadiria hali kudhibitisha kwamba unatekeleza wajibu wake la sivyo uondoke mara moja.

Katika mahojiano ya BBC Dr Bourhan Ghalioun ambaye ni mkuu wa baraza la upinzani amesema ujumbe huo ulishindwa kutoa wazi ukatili wa utawala akitaka shughuli yao nchini kusimamishwa na kukubalia ujumbe maalum kutoka Umoja wa Mataifa.

Dr. Ghalioun ametaka pia nchi za magharibi kusaidia kuweka eneo salama pamoja na kupiga marufuku ndege kupaa anga ya Syria. Ametaka kuwepo na mikakati ya kufanikisha mapinduzi.