Waziri wa Uingereza azuru Burma

Waziri wa masuala ya kigeni wa Uingereza anayezuru Burma amesema kuwa amehakikishiwa na viongozi wa nchi hiyo kwamba watawaachilia huru wafungwa zaidi wa kisiasa.

Akizungumza baada ya kufanya mashauriano na waziri wa nchi hiyo wa masuala ya kigeni mjini Rangoon, William Hague amesema kuwa utawala huo pia umeahidi kwamba harakati za kufanyia mabadiliko mfumo wa kisiasa hazitasitishwa.

Ziara hii ya Hague ambayo ndiyo ya kwanza kwa waziri wa masuala ya Kkigeni kutoka Uingereza katika kipindi cha miaka hamsini inalenga kushinikiza kufanyika kwa uchaguzi huru na wa haki.

Hague anatarajiwa kufanya mashauriano na Rais Thein Sein na kiongozi wa kidemokrasia Aung San Suu Kyi.