Kenya - Sita wauawa katika machafuko

Takriban watu sita ikiwemo watoto watatu wameuawa katika mapigano mapya kati ya jamii mbili hasimu katika jimbo la Moyale kaskazini mwa Kenya.

Machafuko hayo yanaydaiwa kuchochewa na tofauti juu ya maeneo ya kulishia mifugo yametokea katika eneo lilo karibu na mpaka wa Kenya na nchi jirani ya Ethiopia.

Mamia ya watu wameripotiwa kulikimbia eneo hilo na kutafuta hifadhi katika maeneo salama.