Wachuuzi wapambana na polisi Malawi

Watu 30 wamekamatwa kufuatia mapigano kati ya polisi na wafanyabiashara wa mitaani katika mitaa ya mji mkuu wa Malawi, Lilongwe.

Polisi walirusha mabomu ya machozi na kutumia risasi ya mpira kutawanya mamia ya wafanyabiashara hao waliokasirishwa baada ya vibanda vyao kuvunjwa.

Magari yalirushiwa mawe na maduka kadhaa, mengi kati yao yanayomilikiwa na Wachina na Wahindi yalifanyiwa uporaji.

Hali ya utulivu ilirejea baada ya jeshi kuitwa.