ANC yaadhimisha miaka 100

Takriban viongozi arobaini wa mataifa kutoka kote duniani wanatarajiwa kuwasili nchini Afrika Kusini kwa sherehe za kuadhimisha miaka mia moja tangu kubuniwa kwa chama tawala cha African National Congress, ANC.

Zaidi ya watu laki moja pia wanatarajiwa kukongamana katika mji wa Bloemfontein ambako chama hicho kilianzia mwaka 1912.

Chama hicho ni kikongwe zaidi barani Afrika katika vyama vya vita vya ukombozi wa mataifa barani.

ANC Kinasifiwa sana kwa kung'oa mamlaka ya mzungu na kuondoa sera ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Pia kimepongezwa sana kwa kufanya uchaguzi wa kidemokrasia mwaka 1994 na kuandika mojawepo wa katiba huru zaidi duniani.