10 wauawa katika shambulio Nigeria

Watu wasiopungua 10 wameuawa na watu walioficha nyuso zao na kushambulia ukumbi wa umma mjini Mubi kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wakazi wa Mubi wameiambia BBC kuwa waliouawa ni watu wa kabila la Igbo wanaotoka kusini mwa nchi hiyo.

Watu hao walikuwa kwenye mkutano wakupanga jinsi ya kusafirisha mwili wa ndugu yao aliyepigwa risasi na watu wenye silaha siku ya Ahlamisi jioni.

Mji wa Mubi upo katika jimbo la Adamawa, linalopakana na jimbo la Borno, ambapo wapiganaji wa kundi la Waislam wenye itikadi kali walianzisha harakati zao mwaka 2010.