Waandamanaji katika nchi za kiarabu wasifiwa

Waandamanaji katika ncji za kiarabu Haki miliki ya picha AP

Kwenye ripoti yake kuhusu maandamano yaliyoshuhudiwa katika nchi za kiarabu mwaka 2011, shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu {Amnesty International} limewamiminia sifa waandamanaji katika nchi hizo na kusema wametekeleza mageuzi muhimu ambayo jamii ya kimataifa ilishindwa.

Shirika hilo limesema wanaharakati hawataridhia mageuzi finyu ambayo hatoi taswira mpya ya mageuzi kamili. Aidha limesema misimamo ya Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Ulaya na ile ya nchi za Kiarabu haikufanikiwa kuleta mabadiliko na ilikuwa inayumba.

Amnesty International limesema jamii ya kimataifa ilikuwa na misimamo tofauti dhidi ya hali yya haki za binadamu katika mataifa yaliyoshuhudia maandamano ya kutaka mageuzi ya kidemokrasia.

Ripoti hiyo imesema mageuzi ya kidemokrasia katika nchi za Tunisia, Misri na Libya yanafaa kulindwa huku likisema hali nchini Syria ni ile ya kuwakandamiza na kuwaua wapinzani wa serikali ili watawala waendelee kusalia madarakani.