Marekani yaonya Iran kutofunga njia ya mafuta

Waziri wa ulinzi wa Marekani, Leon Panneta ameionya tena Iran dhidi ya jaribio la kufunga kito cha Hormuz kinachotumiwa kama njia ya kusafirishia mafuta kutoka eneo la Ghuba.

Katika mahojiano na runinga ya Marekani, bw. Panneta amesema hatua kama hiyo haitakubaliwa na Marekani.

Iran imetishia kufunga njia hiyo ikiwa itawekewa vikwazo dhidi ya mradi wake wa nyukilia.

Mkuu wa Majeshi ya Marekani Jenerali Martin Dempsey amesema Iran inauwezo wa kfunga njia hiyo, lakini akasema Marekani itazima jaribio kama hilo.