Watu 25 wauawa nchini Afghanistan.

Maafisa Kaskazini Magharibi mwa Pakistan wanasema takriban watu 25 wamuawa na wengine zaidi ya 50 kujeruhiwa katika shambulio la bomu karibu na mpaka wa nchi hiyo na Afghanistan.

Bomu lililotegwa ndani ya gari lililipuka katika soko la Jamrud karibu na kituo cha basi na kulipua magari yaliyokuwa yakitumiwa na waamgambo wanaounga mkono serikali ya nchi hiyo.

Bado haijulikani nani aliyeteklza shambulio hilo.

Eneo la Kaskazini magharibi mwa Pakistan ni ngome ya wanamgambo wa Taleban, al-Qaeda na wanamgambo wengine wanaopinga serikali.