Marekani inataka vikazo zaidi-Iran

Waziri wa fedha wa Marekani, Timothy Geithner, ametoa wito kwa viongozi wa Uchina kusaidia Marekani katika juhudi za kuongeza vikwazo dhidi ya Iran kutokana na mradi wake wa nuklia.

Hata hivyo hakukuwa na ishara yoyote kuwa Uchina iko tayari kubadili msimamo wake kuhusu Iran kuwekwa vikwazo zaidi.

Baada ya mazungumzo hayo mjini Beijing, viongozi hao wanamatumaini kuwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili utaimarika.

Geithner amesma Marekani na Uchina zina uhusiano mwema katika maswala ya ukuaji wa uchumi,maswala ya kifedha na nuklia.

Uchina hutegemea sana mafuta kutoka nchini Iran na imeunga mkono azimio na umoja wa mataifa linaloitaka Iran isitishe mpango wa kurotubiha madini ya Uraniam.