Jamii ya Kimataifa yalaumiwa

Ripoti iliyotolewa na mashirika mawili ya kutoa misaada kutoka Uingereza, inasema kuwa maelfu ya watu walifariki na milioni ya Dola kupotea kwa sababu ya jamii ya kimataifa ilichelewa kuchukua hatua za haraka kufuatia onyo kuwa ukame ulitarajiwa eneo la Afrika Mashariki.

Mashirika ya Oxfam na Save the Children yanasema kuwa mashirika ya kutoa misaada yalichukua muda wa zaidi ya miezi sita kabla ya kuchukua hatua za kukabiliana na janga la njaa lililotokana na ukame, baada ya kupokea onyo.