Ikulu ya White House yarushiwa bomu

Watu wamehamishwa kwa muda kutoka kwa Ikulu ya White Hosue nchini Marekani baada ya bomu ya kutoa moshi kurushwa ndani ya ua la jengo hilo.

Ripoti zinasema kuwa jengo hilo ambalo ni ofisi ya rais Barrack Obama, ilifungwa kwa muda huku maafisa wa idara ya uchunguzi nchini humo CIA, wakifanya uchunguzi kufuatia uvumbuzi wa kifaa killichoonekana kuwa bomu la kutoa moshi.

Msemaji wa idara hiyo ya ujasusi George Ogilvie, amesema kuwa kifaa hicho kilirushwa kupitia ua la jengo hilo wakati waandamanji wapatao 1500 walikuwa wakiandamana nje ya Ikulu hiyo ya rais.