Ocampo kuwasilisha ushahidi zaidi

Mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama ya kimataifa ua Jinai ICC Luis Moreno Ocampo anasema atawasilisha ushahidi zaidi kutaka mashtaka yathibitishwe dhidi ya wakenya wawili mashuhuri, ambao majaji katika mahakama hiyo waliamua kukataa kuthibitisha mashtaka dhidi yao kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini humo.

Siku ya jumatatu mahakama ya ICC ilithibitisha mashtaka dhidi ya washukiwa wanne, akiwemo naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta, lakini majaji wakasema hawakuridhishwa na ushahidi ulitololewa na kiongozi wa mashtaka dhidi ya aliyekuwa mkuu wa Polisi Meja Jenerali Hussein Ali na waziri wa zamani Henry Kosgey na kwa hivyo wakakataa kuthibitisha mashtaka dhidi yao.