Kamanda wa al-qaeda auwawa Yemen

Ripoti kutoka Yemen zinasema kuwa wapiganaji kumi na watatu wa mtandao wa kigaidi wa al Qaeda, wameuawa kwenye shambulio la anga lililotekelezwa na ndege za jeshi la Marekani katika mkoa wa Abyan.

Maafisa wa serikali wanasema wengi wa wale waliouawa walikuwa wakihudhuria mkutano katika jengo moja.

Mmoja wao anasemekanaa kuwa kamanda mkuu wa kundi hilo al Qaeda katika eneo hilo.

Maafisa wa ulinzi wa Yemen wanasema, mashambulio hayo yalitekelezwa na ndege za marekani zizizokuwa na rubani.

Wanamgambo wa kiislamu wanathibiti sehemu kubwa ya mkoa huo wa Abyan kufuatia mzozo wa kisiasa uliodumu kipindi cha miezi kadhaa nchini Yemen.